Select your language

Timu za Mpira wa Wavu ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Wanaume na Wanawake zimeshiriki ufunguzi wa Ligi ya Mpira wa Wavu Taifa -Tanzania Volleyball National League (TVNL) uliofanyika katika viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam. 

‎Kocha wa timu hizo Bw.Willy Barton amesema kuwa vikosi vyake vipo tayari kwa ligi hiyo na kuwahakikishia Menejimenti ya TPA, Mashabiki na Wadau, ushindi katika mechi zote na hatimaye kunyakuwa ubingwa wa michuano hiyo. 

‎Aidha Timu ya Mpira wa wavu ‎wanawake ya TPA,  tarehe 26 Julai 2025  itaingia dimbani dhidi ya Jeshi Stars katika mchezo utakaochezwa katika viwanja vya Mwembe Yanga Jijini Dar es Salaam.
‎ 
‎Ligi ya Mpira wa Wavu Taifa imeandaliwa na Chama cha mpira wa Wavu Tanzania  (TVF)  ikishirikisha timu 14 kwa Wanaume na kwa upande wa Wanawake ni timu  7 ambapo ligi hiyo itaanza rasmi kuchezwa tarehe 26 Julai  hadi Agosti 1, 2025.