“THE EXTRA MILE "BANDARI YA TANGA YAWEKA MKAZO KATIKA HUDUMA BORA KWA WATEJA
Bandari ya Tanga imevuka malengo ya utendaji kwa mwaka wa fedha 2025/2026 baada ya kuhudumia meli 616 dhidi ya lengo la meli 360 pamoja na tani milioni 2.179 za shehena ikiwa ni juu ya lengo la kuhudumia tani milioni 1.65.
Hayo yamebainishwa na Meneja wa Bandari ya Tanga Bw. Salehe Mbega alipokuwa akiongea na wadau wa bandari hiyo kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026 katika jengo la “ Bandari House”
Mbega alisema kuwa mafanikio yanayoonekana katika bandari hiyo yamechangiwa na ushirikiano kati ya TPA, wateja na wadau mbalimbali wa bandari.
Aidha alieleza kuwa maboresho yaliyofanyika bandarini hapo katika kuhudumia meli na mizigo ya wateja yamepunguza kwa kiasi kikubwa malalamiko ya wateja kutokana na utendaji kazi wenye ufanisi mkubwa.
Akitoa neno la shukrani kwa TPA, Meneja wa Wakala wa Meli wa Seafront Shipping Bw. Amri Kaghembe amepongeza huduma inayotolewa na Bandari ya Tanga akisema dhana ya ‘The Extra Mile’ inaonekana kwa vitendo.
“Huduma bora kwa mteja haipaswi kutolewa kwa sababu ni wajibu pekee, bali ni kutambua mteja anastahili huduma bora”. Aliongeza Kaghembe.
katika kutambua umuhimu wa wateja Bandari ya Tanga inawashukuru wateja na wadau wote kwa ushirikiano wao huku ikiahidi kuendelea kuboresha huduma na kwenda hatua ya ziada ‘The Extra Mile’ katika kuhudumia wateja.Bandari ya Tanga imevuka malengo ya utendaji kwa mwaka wa fedha 2025/2026 baada ya kuhudumia meli 616 dhidi ya lengo la meli 360 pamoja na tani milioni 2.179 za shehena ikiwa ni juu ya lengo la kuhudumia tani milioni 1.65.
Hayo yamebainishwa na Meneja wa Bandari ya Tanga Bw. Salehe Mbega alipokuwa akiongea na wadau wa bandari hiyo kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026 katika jengo la “ Bandari House”
Mbega alisema kuwa mafanikio yanayoonekana katika bandari hiyo yamechangiwa na ushirikiano kati ya TPA, wateja na wadau mbalimbali wa bandari.
Aidha alieleza kuwa maboresho yaliyofanyika bandarini hapo katika kuhudumia meli na mizigo ya wateja yamepunguza kwa kiasi kikubwa malalamiko ya wateja kutokana na utendaji kazi wenye ufanisi mkubwa.
Akitoa neno la shukrani kwa TPA, Meneja wa Wakala wa Meli wa Seafront Shipping Bw. Amri Kaghembe amepongeza huduma inayotolewa na Bandari ya Tanga akisema dhana ya ‘The Extra Mile’ inaonekana kwa vitendo.
“Huduma bora kwa mteja haipaswi kutolewa kwa sababu ni wajibu pekee, bali ni kutambua mteja anastahili huduma bora”. Aliongeza Kaghembe.
katika kutambua umuhimu wa wateja Bandari ya Tanga inawashukuru wateja na wadau wote kwa ushirikiano wao huku ikiahidi kuendelea kuboresha huduma na kwenda hatua ya ziada ‘The Extra Mile’ katika kuhudumia wateja.


EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"