Select your language

Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inaratibu mpango wa ujenzi wa gati mpya zipatazo 10 ili kuhudumia meli nyingi zaidi kwa wakati mmoja.

 

Kauli hiyo imetolewa katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni leo  tarehe 13 Aprili,2026 na Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe.David Kihenzile, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Amina Ali Mzee.

 

Mbunge huyo alitaka kujua mpango wa Serikali  wa kuongeza gati katika Bandari ya Dar es salaam ili kuiwezesha kuhudumia meli nyingi zaidi.