PIC YAIPONGEZA BANDARI YA DAR ES SALAAM KWA UFANISI.
Kamati ya Maboresho ya Bandari ( PIC) iliyokutana Oktoba 23,2926 katika kikao chake cha kila mwezi, imepongeza ufanisi na mafanikio makubwa yaliyofikiwa na Bandari ya Dar es Salaam katika uhudumiaji wa shehena kwa mwaka wa fedha wa 2025/2026.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Kikao cha Kamati hiyo, Prof.Godius Kahyarara alisema Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania ( TPA) kwa kushirikiana na Waendeshaji binafsi wa Bandari kupitia uwezeshaji wa Serikali.
Prof Kahyarara alisema kwa pamoja wamefanyakazi kubwa inayonasibishwa na namba za ukubwa wa shehena iliyohudumiwa na kupelekea kuvukwa kwa malengo yaliyowekwa kwa mwaka wa fedha uliopita 2025/2026.
Awali akitoa taarifa ya utendaji wa Bandari ya Dar es Salaam kikaoni hapo, Mkurugenzi wa Bandari hiyo Bw.Gallus Abed Gallus alisema uwezo wa kuhudumia shehena umeongezeka hali iliyopelekea kuvuka lengo la uhudumiaji shehena kwa asilimia 23.


EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"