Select your language

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila, amemuagiza Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Abdul Mhinte kuunda timu ya wataalamu kutoka Sekta za Umma na Binafsi katika Mkoa wa Dar es Salaam ili kutafuta suluhu ya kudumu ya msongamano wa malori na magari mengine katika Jiji la Dar es Salaam. 



‎Mhe. Chalamila ametoa maagizo hayo tarehe 11 Julai, 2025 alipokutana na viongozi waandamizi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Wadau wa Sekta za Umma na Binafsi wanaohusika katika sekta ya Uchukuzi na Menejiment ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).



‎Aidha, Mhe. Chalamila amewataka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini  (TARURA) na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kushirikiana na Jeshi la Polisi kuhakikisha wanaondoa malori yote yanayoegeshwa kando ya Barabara, hususan barabara zinazoingia na kutoka Bandarini.