MICHEZO YA BANDARI 2026 YATIKISA MOROGORO KWA SHANGWE NA HAMASA
Timu mpira wa wavu za Bandari ya Mtwara wanawake na wanaume zimefanikiwa kutika fainali ya Michezo ya Bandari 2026 inayoendelea mjini Morogoro.
Timu ya Wavu ya Wanaume ilifanikiwa kutinga hatua hiyo baada kuishinda timu Makao Makuu kwa seti 2-0) huku ile ya wanawake ikifanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kumfunga bingwa mtetezi Bandari ya Dar es Salaam kwa seti 2-0 katika mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa.
Katika mpira wa Kikapu Bingwa mtetezi Bandari ya Tanga aliifunga timu ya Makao Makuu jumla ya vikapu 66 -39 katika mchezo uliokuwa wa upande mmoja.
Katika mchezo wa Netiboli timu ya Bandari ya Zanzibar iliishinda Bandari Tanga jumla ya magoli 40 -26.
Kwa upande wa michezo ya Jadi Bi Nezia Daudi ameibuka bingwa wa drafti,Salma Khalid wa Bandari ya Dar es Salaam akijinyakulia taji la bingwa wa karata kwa uoande wa wanawake huku Cartace Ngajiro wa Bandari wa Tanga amebuka Bingwa wa bao kwa upande wa Wanawake.
Kwa upande wa Wanaume Mohamed Hamad wa Bandari ya Zanzibar amekuwa mshindi katika mchezo wa karata na James Mandawa kutoka Bandari za Ziwa Tanganyika ameibuka bingwa wa mchezo wa bao.



EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"