MENEJIMENTI YA BANDARI DAR ES SALAAM KUBOLESHA UFANISI NA UTENDAJI KAZI BANDARINI
Menejimenti ya Bandari ya Dar es Salaam, Februari 16, 2026 imefanya kikao cha siku moja na wadau mbalimbali wa sekta ya bandari kwa lengo la kujadili masuala muhimu yanayohusu uboreshaji wa huduma na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi bandarini.
Kikao hicho kimewaleta pamoja wadau wakuu wanaohusika katika mnyororo wa huduma za bandari, ambapo pamoja na mambo mengine, walijadiliana changamoto zilizopo na kuweka mikakati ya kupata ufumbuzi wa kudumu ili kuongeza kasi ya utoaji huduma na kurahisisha shughuli za biashara.
Baadhi ya wadau waliohudhuria ni pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), DP World Dar es Salaam LTD, Tanzania East Africa Gateway Terminal (TEGTL), Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA),Chama cha Mawakala wa Meli Tanzania (TASAA), Chama cha Wamiliki wa Bandari Kavu Tanzania (CIDAT), Tanzania Customs Agents Association (TACAS), Chama cha Waondoshaji na Wapelekaji Shehena Bandarini na Mipakani Tanzania (TAFFA) pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama na taasisi nyinginezo.
Kikao hicho kimeongozwa na Meneja Zimamoto na Usalama, Bw. Mussa Biboze, kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Abed Gallus Abed.
Menejimenti ya bandari ya Dar es Salaam, imesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa karibu kati ya wadau wote ili kuhakikisha huduma zinaboreshwa, muda wa kuhudumia mizigo unapungua na bandari inaendelea kuwa lango kuu la biashara kwa Tanzania na nchi jirani.


EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"