Select your language

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Juni 28, 2026 imeandika historia mpya baada ya kufanikiwa kwa mafanikio makubwa operesheni ya kuzamisha Kizimba Maalum kinachoelea kwa ajili ya matengenezo ya meli (Floating Dock) hadi kufikia kiwango chake cha juu cha kuzama majini (Maximum Operating Draft) katika Bandari ya Dar es Salaam. Hatua hii muhimu ni sehemu ya maandalizi ya kuanza rasmi huduma za kisasa za ukarabati na matengenezo ya meli hapa nchini kupitia Floating Dock yenye uwezo wa kubeba Meli yenye uzito wa hadi tani 1,500.Mradi huo ambao umefikia asilimia 98 ya utekelezaji wake utawezesha:
✅ Matengenezo ya meli kufanyika nchini
✅ Kuokoa fedha za kigeni
✅ Kuongeza ajira na ujuzi kwa Watanzania
✅ Kuimarisha uchumi wa buluu
✅ Kuiweka Tanzania kuwa kitovu cha huduma za ukarabati wa meli Afrika Mashariki na Kati .Mafanikio haya yametokana na ushirikiano, weledi na kujituma kwa timu nzima iliyoshiriki katika utekelezaji wa mradi huu wa kimkakati.TPA inaendelea kuimarisha miundombinu ya bandari kwa viwango vya kimataifa kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa huduma za usafirishaji wa majini nchini.