MADIWANI WA KILOMBERO WAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA UWEKEZAJI MKUBWA BANDARI YA TANGA
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero wamempongeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uwekezaji mkubwa uliofanyika katika Bandari ya Tanga.
Baraza hilo limetoa pongezi hizo wakati walipotembelea Bandari ya Tanga kwa ziara ya mafunzo wa shughuli za bandari. Katika pongezi hizo wamesema, Mhe. Rais ameifungua Bandari ya Tanga na kuzivutia nchi za jirani kuitumia bandari hiyo katika kuagiza na kusafirisha bidhaa mbalimbali.
Awali akiwakaribisha Madiwani hao, Meneja wa Bandari, Bw. Salehe Mbega alisema maboresho yaliyofanyika yalikuwa na lengo la kuijengea uwezo Bandari katika kuhudumia meli kubwa gatini, kuhudumia shehena kubwa ya mzigo na kukusanya mapato zaidi.
Aidha Bw. Mbega alisema maboresho makubwa yaliyofanyika yamefungua fursa ya uwekezaji katika bandari kavu na maghala ya kuhifadhia mizigo ya wateja. Ametoa rai kwa wawekezaji kuchangamkia fursa hizo.


EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"