MAAFISA NA WANAFUNZI WA CHUO CHA CSC WATEMBELEA BANDARI KAVU YA KWALA KWA ZIARA YA KIMAFUNZO
Maafisa Waandamizi Wakufunzi na Wanafunzi (45) kutoka Chuo cha Mafunzo ya Ukamanda na Unadhimu Tanzania (CSC) cha Duluti Mkoani Arusha, tarehe 13 Oktoba,2026 wamefanya ziara ya kimafunzo katika Bandari Kavu ya Kwala, Kibaha Pwani.
Ujumbe huo uliongozwa na Kanali Jackson Mwakalinga umejumuisha Maafisa wa kijeshi kutoka mataifa ya Burundi, Namibia, Botswana, Zimbabwe, Zambia, Sierra Leone, India na wenyeji Tanzania.
Ziara hiyo inalenga kujifunza shughuli za Bandari pamoja na kuwajengea uelewa wa namna maendeleo ya kiuchumi yanavyochangia kuimarisha ulinzi na usalama wa Taifa.
Ujumbe huo ulipokelewa na Meneja wa Makasha Bw. Geofrey Lwesya kwa niaba ya Mkurugenzi wa Bandari Bw. Abed Gallus Abed.


EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"