KATIBU MKUU WA WIZARA YA UCHUKUZI AFUNGUA KONGAMANO LA KITAIFA LA WADAU WA UCHUMI WA BULUU 2025 JIJINI DAR ES SALAAM

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imekuwa ikichangia maendeleo ya Uchumi wa Buluu kupitia uendelezaji na ujenzi wa Bandari za mwambao wa Bahari na maziwa makuu nchini.
Kauli hiyo imetolewa Septemba 11, 2025 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara, wakati akifunga Kongamano la Kitaifa la Wadau wa Uchumi wa Buluu 2025, lililofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam.
Katika hotuba yake Prof. Kahyarara amesema, Serikali kupitia TPA imefanya maboresho katika bandari zake za Dar es Salaam, Tanga, Mtwara pamoja na za Ziwa Nyasa, Victoria na Tanganyika, ili kuchochea maendeleo ya Uchumi wa Buluu.
Aidha Prof.Kahyarara amesema, Bandari zilizoko kwenye maziwa zinaunganisha nchi yetu na nchi zisizo na bahari kupitia usafirishaji wa shehena kwa njia ya maji.
Amesema kwa maboresho yaliyofanyika katika Bandari ya Dar es Salaam, Bandari hiyo inaenda kuwa kivutio zaidi na chaguo kwa Wateja, katika Ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara.