DKT. BARAKA MDIMI AONGOZA KIKAO CHA 16 CHA BARAZA DOGO LA MAJADILIANO LA MAKAO MAKUU.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mha. Dkt. Baraka R. Mdima ameongoza kikao cha (61) cha Baraza Dogo la Majadiliano la Makao Makuu (JIC) kinachofanyika Mjini Bagamoyo.
Kikao hiko kimelenga kujadili mambo mbalimbali ya kiutendaji katika kuboresha huduma na miundombinu ya bandari ili kuongeza ufanisi wa huduma za Mamlaka.
Pamoja na mambo mengine Baraza hilo limemuaga na kumtakia kheri aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Shughuli za Meli na Bandari Tanzania (DOWUTA) Tawi la Makao Mkuu (HQ) Bw. Benjamin Kihanga aliyemaliza muda wake wa Utumishi kisheria.


EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"