BARAZA LA MAJADILIANO (CJIC) LA TPA LIMEFANYA KIKAO CHA KAWAIDA JIJINI MOROGORO

Baraza kuu la Majadiliano (CJIC) la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) limefanya kikao cha kawaida cha Hamsini na Saba (57) kinachofanyika mjini Morogoro.
Kikao hiko kimelenga kupitia na kuthibitisha Utekelezaji wa Makubaliano ya Kikao cha kawaida cha Hamsini na sita (56) kilichofanyika Disemba 2024.
Pamoja na mambo mengine, Baraza hilo limewaaga wajumbe wake ambao ni Afisa Mwandamizi Bandari ya Kyela Bw. Florian Mloka na Katibu wa DOWUTA Tawi la Dar es Salaam Bw. Hassan Ahmed kwa kuhitimisha muda wa wao wa utumishi kisheria katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).