BARAZA KUU LA WAFANYAKAZI WA TPA LIMEFANYA KIKAO CHA THELATHINI NA NANE (38) JIJINI MOROGORO

Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) leo tarehe 03 Septemba 2025 limefanya kikao cha Thelathini na nane (38) kilichofanyika mjini Morogoro.
Kikao hiko cha siku mbili kimelenga kujadili na kupokea utekelezaji wa bajeti kwa mwaka 2024/2025 na mpango na bajeti kwa mwaka 2025/2026.
Baraza hilo limeongozwa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala Bw. Mbarikiwa Y. Masinga kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bw.Plasduce M. Mbossa.