Select your language

Bandari ya Tanga imekuwa ni kiungo muhimu cha shughuli za kiuchumi katika Mkoa wa Tanga, Mikoa jirani pamoja na nchi jirani zinazotuzunguka.Kauli hiyo imetolewa na Afisa Biashara Mkoa wa Tanga Bw. Peter Lyochi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Dkt . Balozi Batilda Buriani kwenye kilele cha maadhimisho ya 13 ya Biashara na Utalii ya Mkoa huo yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwahako.Bw. Lyochi alisema kuwa uwepo wa bandari iliyoboreshwa imewapa wadau nafasi ya kupeleka bidhaa nje ya nchi. “Exports” na kupokea “imports” kwa urahisi .“Bandari ya Tanga pia imefanikisha uamuzi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga hatua hii imetoa fursa za ajira na itaongeza pato la Taifa” Aliongeza Lyochi.Maonesho ya 13 ya Biashara na Utalii Tanga huandaliwa na Chemba ya Taifa ya Biashara Tanzania (TNCC) ambapo Bandari ya Tanga hushiriki na kutumia jukwaa hilo kutoa elimu na kutoa taarifa juu ya utendaji kazi wenye ufanisi.