Select your language

Meneja wa Bandari ya Tanga, Bw. Salehe Mbega, amewataka Wadau wa Bandari hiyo kuendelea kushirikiana katika kutoa huduma bora kwa wateja wanaotumia bandari hiyo ili kuvutia wateja zaidi.

Meneja huyo ametoa rai hiyo wakati wa kikao cha Wadau wa Bandari ya Tanga cha mwezi Oktoba 2026 kilichofanyika Jijini Tanga katika ukumbi wa Bandari House.

Vikao hivyo vya Bandari hufanyika kila mwezi vikiwa na lengo la kujadili changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika utoaji huduma kwa wateja ili kuzitafutia ufumbuzi wa pamoja.