BANDARI YA DAR ES SALAAM KUHUDUMIA TANI MILIONI 62 ZA SHEHENA KUFIKIA 2031
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Abed G. Abed, tarehe 9 Oktoba 2026 katika hafla fupi ya kufunga Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa Kituo cha Bandari ya Dar es Salaam iliyofanyika katika Viwanja vya Kitengo cha Zimamoto na Usalama Bandari ya Dar es Salaam.
Amesema hapo awali mipango ilikuwa kuhudumia tani milioni 30 ifikapo mwaka 2030 lakini kutokana na ufanisi mkubwa, Bandari ya Dar es Salaam imehudumia jumla ya tani milioni 33.7 na kuelezea kuwa mipango ya sasa ni kuhudumia shehena tani Milioni 62 kufikia mwaka wa fedha 2030/2031.
Ili kufikia malengo hayo amewaasa Wafanyakazi kutofanya kazi kwa mazoea kwa kujituma zaidi, kuwa waadilifu na kuongeza ubunifu katika kuwahudumia wateka.
Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Mwaka 2026 ni “The Extra Mile”.


EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"