BANDARI YA DAR ES SAALAM YATALAJIA KUHUDUMIA TANI MIL 33 MWISHO WA MWAKA WA FEDHA 2025/2026
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Abed G. Abed alipozungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Bw. Plasduce M. Mbossa , tarehe 26 Juni 2026, alipokutana na Wanakwaya wa Kwaya ya Walimu ya Jiji la Mwanza pamoja na Uongozi wa Shirikisho la Walimu Nyamagana, Mwanza katika ziara ya mafunzo. Bw. Gallus amesema kwamba ongezeko hilo la shehena tarajiwa linatokana uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam ambao umekuwa na manufaa makubwa kwa kuwa ukilinganisha na miaka ya nyuma kabla ya uwekezaji huo kufanyika
Bw. Gallus amesema kwamba awali lengo la Bandari ya Dar es Salaam lilikuwa kuhudumia shehena tani milioni 30 ifikapo mwaka 2030 lakini baada ya uwekezaji kwa kushirikiana na Sekta binafsi , Bandari ya Dar es Salaam imefikia lengo hilo kwa Mwaka wa fedha 2025/2026 .Mkurugenzi huyo amebainisha kuwa jumla ya shehena iliyohudumiwa katika kipindi cha miezi 11 mwaka wa fedha 2025/26 ni tani Milioni 30.8 ambapo matarajio ndani ya mwezi mmoja uliobaki Bandari itahudumia zaidi ya tani milioni 2.9 hivyo mpaka kufikia mwisho wa mwaka wa fedha 2025/ 2026 Bandari itahudumia Shehena tani 33. 7 ikilinganishwa na milioni 27.7 iliyohudumiwa kipindi kama hicho mwaka wa fedha 2024/2025 Ikiwa ni ongezeko la tani Milioni 6 ndani ya mwaka mmoja.Kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Bandari ya Dar es Salaam ilihudumia Tani milioni 23.7 lakini mwaka mmoja baadae mwaka wa fedha 2024/2025 ilihudumia Shehena tani milioni. 27.7 ikiwa ni ongezeko la Tani milioni 4 . Ziara hiyo ya Wanakwaya na Shirikisho ilikuwa na lengo na kujifunza juu ya maboresho yaliyofanyika Bandari ya Dar es Salaam na ufanisi uliofanyika kutokana na hatua hizo, ambapo wameipongeza Serikali kwa kuongeza uwezo wa bandari.
EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"