Select your language

Balozi wa Urusi hapa nchini Mhe. Andrey Avetisyan, ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa kuendelea kuiboresha Bandari ya Mtwara, inayoendelea kutoa huduma bora na za ufanisi. 

Balozi Avetisyan, ametoa pongezi hizo, tarehe 8 Septemba, 2025 alipofanya ziara ya kutembelea Bandari ya Mtwara, ambapo ameongozana na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali Patrick Kenan Sawala pamoja viongozi mbalimbali wa ngazi ya Mkoa.

Amesema pia ameridhishwa na utendaji kazi wa Bandari ya Mtwara, na kueleza kubaini fursa mbalimbali zilizopo katika Bandari hiyo, ambazo zikitumiwa vizuri zitaleta maendeleo na ongezeko la mapato zaidi. 

Kwa upande wake, Meneja wa Bandari ya Mtwara Bw. Ferdinand Nyathi,  ameelezea hali ya utendaji kazi wa Bandari hiyo kuwa umeimarika zaidi , kufuatia maboresho mbalimbali yaliyofanywa na Serikali ambayo yameongeza tija na ufanisi katika utoaji wa huduma.

Uchaguzi 2025 Logo