BALOZI WA DENMARK NCHINI AKUTANA NA MENEJIMENTI YA TPA
Serikali ya Denmark imeonesha nia ya kuimarisha ushirikiano na Tanzania katika kukuza biashara na uwekezaji kwenye sekta ya uchukuzi kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).
Balozi wa Denmark nchini, Mhe. Jesper Kammersgaard, ameeleza Serikali yake kuvutiwa na maendeleo ya Bandari ya Dar es Salaam pamoja na mwelekeo wake wa kimkakati wakati wa kikao na Menejimenti ya TPA kilichofanyika Aprili 30, 2026.
Kwa upande wa TPA, Naibu Mkurugenzi Mkuu, Mha. Dkt. Baraka Mdima amesema uwezo wa kuhudumia shehena umeongezeka maradufu, hali iliyochochea ongezeko la meli bandarini.
TPA pia inaendelea na mipango ya kuendeleza bandari za kimkakati kama Mbegani Bagamoyo na Bandari Kavu ya Kwala ili kuimarisha mtandao wa usafirishaji kwa reli na barabara, na kupunguza msongamano katika Bandari ya Dar es Salaam.


EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"