BAANDARI YA DAR ES SALAAM YAFANIKIWA KUTETEA UBINGWA WA JUMLA KATIKA MICHEZO YA BANDARI 2026
Bandari ya Dar es Salaam imefanikiwa kutetea Ubingwa wa Jumla katika michezo ya Bandari 2026 iliyomalizika leo Mkoani Morogoro kwa tofauti ya Alama 1 kwa uwiano wa Medali dhidi ya Bandari ya Tanga ambao ushindi wao wa mabao 2 kwa 0 dhidi ya Bandari Zanzibar haujawasaidia kuwapiku Bandari ya Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi katika Michezo hiyo Mkuu wa Wilaya ya MOROGORO Mussa Kilakala kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, ametoa Rai kwa TPA kuirejesha tena Michezo hiyo Mkoani humo kwani inachagiza uchumi.
Bingwa kwa upande wa mpira wa miguu ilikuwa timu ya bandari ya Tanga baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 2 -0 dhidi ya timu ya Bandari ya Zanzibar (ZPC) katika mchezo wa fainali uliopigwa katika uwanja wa Jamhuri.
Nafasi ya tatu ilinyakuliwa na timu ya Bandari ya Dar es Salaam baada ya kuizabau kwa jumla ya magoli 4 - 1 Makao Makuu (HQ) katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu.
Kwa upande wa mchezo wa netiboli timu ya Bandari ya Zanzibar ilinyakua ubingwa wa michuano hiyo huku nafasi ya mshindi wa pili ikienda kwa Bandari ya Dar es Salaam na ya tatu Bandari ya Mtwara.
Mchezo wa Kamba kwa wanamume Bingwa ni Bandari ya Tanga,nafasi ya pili imekwenda kwa Bandari ya Dar es Salaam na mshindi wa tatu ni Bandari ya Zanzibar.
Kamba wanawake safari hii timu tatu zimefungana kwa kunyakua ubingwa zote kwa pamoja, ambazo nk Bandari za Tanga,Dar es Salaam na Makao Makuu.
Katika mchezo wa mpira wa kikapu (Basketball) bingwa ni Bandari ya Tanga,mshindi wa pili Bandari ya Dar es Salaam na wa tatu ni Bandari za Maziwa.
Katika mchezo wa Wavu (Volleyball)wanamume bingwa ni Makao Makuu,mshindi wa pili ni Bandari ya Mtwara na nafasi ya tatu imenyakuliwa na Bandari ya Dar es Salaam.
Mchezo wa mpira wa Wavu Wanawake bingwa ni Bandari ya Dar es Salaam,nafasi ya pili imenyakuliwa na Bandari ya Mtwara huku Bandari ya Tanga ikiweka kibindoni nafasi ya tatu.
Kwa upande wa michezo ya jadi,Draft wanamume bingwa ni Bandari ya Tanga na wanawake bingwa ni Makao Makuu,Karata wanawake bingwa ni Bandari ya Dar es Salaam na bao wanaume bingwa ni Bandari za Maziwa na wanawake bingwa ni Bandari ya Tanga.


EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"