Sélectionnez votre langue

Bandari ya Mtwara imeendelea kupongezwa kwa utendaji kazi wenye ufanisi mkubwa na tija katika kuhudumia shehena mbalimbali za ndani na nje ya Nchi.

Pongezi hizo zimetolewa tarehe 11 Disemba 2025, na Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo (Mb.), wakati wa ziara yake ya kutembelea Bandari ya Mtwara.

Mhe. Chongolo ameonesha kuridhishwa na hali nzuri ya miundombinu, mitambo na vitendea kazi vya kisasa, ambavyo vyote ni matokeo ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika kuboresha uwezo wa bandari hiyo.

Kwa upande wake, Meneja wa Bandari ya Mtwara, Bw. Ferdinand Nyathi, amesema kuwa bandari hiyo inaendelea kuhudumia shehena ya korosho kwa ufanisi mkubwa pamoja na shehena nyingine mbalimbali. Ameongeza kuwa muda wa wastani wa kuhudumia meli na shehena umepungua kutoka siku 7 hadi siku 4, hatua inayoonesha maboresho makubwa ya kiutendaji.