WAFANYAKAZI BANDARI YA TANGA WAASWA KUENDELEA KUIMARISHA UWAJIBIKAJI
Wito umetolewa kwa wafanyakazi wa Bandari ya Tanga kuendelea kuimarisha uwajibikaji kwa kushirikiana kulinda mali za Mamlaka, sambamba na kuzingatia nidhamu katika maeneo ya kazi.
Wito huo umetolewa na Meneja wa Bandari ya Tanga, Bw. Salehe Mbega, alipokuwa akifunga Kikao cha 73 cha Baraza la Dogo la Majadiliano (JIC) la kituo hicho, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Bandari House jijini Tanga.
Akizungumza katika kikao hicho, Mbega amesema kuwa mafanikio na maendeleo ya Bandari ya Tanga yanategemea sana ushirikiano, uadilifu na uwajibikaji wa kila mfanyakazi katika kulinda rasilimali za taasisi na mali za wateja.
Katika kuhitimisha hotuba yake, Mbega amewataka wafanyakazi kuimarisha mshikamano na kuzingatia maadili ya kazi kwa manufaa ya Mamlaka na taifa kwa ujumla

EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"