Sélectionnez votre langue

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana Mhe.Joel Arthur Nanauka ametembelea Banda la Bandari ya Mtwara katika maonesho yaliyoshirikisha wadau waliopo kwenye mnyororo wa thamani wa zao la korosho.

 Maonesho hayo yameambatana na Mbio za Korosho Marathon ambazo zimefanyika tarehe 29.11.2025. Mhe.Nanauka ameeleza kuridhishwa na taarifa za hali ya utendaji kazi wa Bandari ya Mtwara kufuatia kuongezeka kwa uwezo wa kuhudumia shehena kutoka Tani milioni 1.7 kwa mwaka hadi kufikia zaidi ya Tani milioni 2.5 kwa mwaka.

Akiwasilisha taarifa hizo, Kaimu Meneja wa Bandari ya Mtwara Bw. Mtunze Sudi ameeleza kuwa kwa sasa Bandari ya Mtwara imeimarisha zaidi huduma zake ambapo inahudumia shehena ya Mafuta ya transit ambayo yanasafirishwa kwenda nchi mbalimbali ikiwemo Malawi, Zambia, Rwanda, DRC na Burundi.