TPA YAPONGEZWA KWA UFANISI
Chama cha Waendesha Bandari Mashariki na Kusini mwa Afrika (PMAESA) kimepongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa ushirikiano inaoutoa kwa taasisi hiyo.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa PMAESA Bw.Mohamed Abdul alipotembelea banda la TPA katika Maonesho yanayokwenda sambamba na Mkutano wa Chama hicho unaofanyika jijini Dar es Salaam.
Alisema PMAESA inatambua mchango na ufanisi wa TPA katika uhudumiaji wa shehena inayopita katika ukanda huu wa Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Wadau mbalimbali wanohudhuria Mkutano huo wa watumiaji wa Bandari wamepata fursa ya kutembelea banda la TPA na kupata ufafanuzi wa masuala yahusuyo bandari za Tanzania.


EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"