Sélectionnez votre langue

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeibuka mshindi wa kwanza wa tuzo ya umahiri katika uandaaji bora wa hesabu za fedha kwa kuzingatia viwango vya uandaaji hesabu vya kimataifa (IFRS) katika tuzo zilizotolewa na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu nchini (NBAA) kwa mwaka wa fedha 2023/2024, zilizofanyika Disemba 4,2025 Jijini Dar es Salaam.