Sélectionnez votre langue

Timu tatu za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) zinazoshiriki mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi nchini (SHIMMUTA) zimefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kushinda michezo yao ya hatua ya robo.

Timu ya Netiboli ilitinga hatua hiyo ya nusu fainali baada ya kuizabua bila huruma timu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) magoli 53 - 32 hiyo ni baada kuwa imeishinda timu Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jumla ya magoli 57 - 20 katika mchezo wa 16 bora.
Timu mbili za mchezo wa kuvutana kwa kamba (wanaume na wanawake) nazo zimetinga hatua ya nusu fainali baada ya kushinda michezo yao ya robo fainali dhidi ya MUHAS kwa wanaume na dhidi ya MNH kwa wanawake, huku timu ya Mpira wa kikapu ikitinga hatua ya robo fainali kwa kuizaba timu ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania TFRA) jumla ya vikapu 52 - 18 na sasa itacheza nusu fainali na timu ya TFS. 

Timu za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ambao ndio mabingwa wa jumla wa michuano iliyopita zimeendelea kufanya vizuri kwa kufanikiwa kuingia hatua ya robo fainali ambazo ni Mpira wa wavu (Volleyball ke na me) ,Mpira wa kikapu (wanawake)