Sélectionnez votre langue

Michezo ya 18 ya Bandari “InterPorts Games 2025” imefungwa rasmi leo mjini Morogoro, huku Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Bw.Plasduce Mbossa, akisisiatiza umuhimu wa watumishi wote wa sekta ya bandari kushiriki kwa wingi katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29.

Maelekezo hayo ya Mkurugenzi Mkuu yametolewa katika hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa TPA, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano hayo, Bw. Mbarakiwa Masinga.

Bandari ya Dar es Salaam imeibuka Mshindi wa jumla wa Michezo hiyo Mwaka 2025 ikiwa ni mara ya tatu mfululizo huku ikinyakua jumla ya vikombe 13 kati ya vikombe vilivyokuwa vinawaniwa na jumla ya timu zilizoshiriki Mashindano hayo.

 Bandari ya Dar ea Salaam imetwaa ubingwa wa Mpira wa Wavu kwa Wanawake na Wanaume, na pia ikiongoza upande wa Riadha mita 1500 na kufuatiwa na Bandari ya Tanga na DP World.

Kwa upande kwa Kandanda timu ya Shirika la Bandari Zanzibar (ZPC) ilinyakua ubingwa baada ya kuilaza Bandari ya Dar es Salaam 1 - 0 katika mchezo wa fainali,huku nafasi ya ushindi wa tatu ikinyakuliwa na Makao Makuu DP World baada ya kuifunga timu ya DP World magoli 4 - 3.

Kwenye Mpira wa Netiboli Timu ya Shirika la Bandari Zanzibar (ZPC) imekuwa mshindi kwa tofauti ya magoli 16 dhidi ya timu ya Bandari ya Dar es Salaam huku Bandari ya Tanga ikitwaa ubingwa wa mchezo wa mpira wa kikapu.

Kwa upande wa mpira wa Wavu Wanawake bingwa ameibuka Bandari ya Dar es Salaam akifuatiwa na Bandari za Mtwara na Tanga.Katika mchezo wa kamba wanaume bingwa ni Bandari ya Tanga,mshindi wa pili ni Shirika la Bandari Zanzibar na mshindi wa tatu ni Bandari ya Dar es Salaam.

Kufuatia matokeo hayo yalishirkisha timu na wachezaji kutoka Makao Makuu ya TPA, Bandari za Dar es Salaam, Tanga, Mtwara na Maziwa, DP World, TACOSHIL na Shirika ka Bandari Zanzibar, Mkurigenzi Mkuu ameipongeza Kamati ya Maandalizi kwa kufanikisha michezo hiyo kwa nidhamu na uadilifu.