Sélectionnez votre langue

Timu za mabingwa wa jumla wa mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni binafsi nchini (SHIMMUTA), Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kama ilivyotarajiwa, zimeanza kibabe kutetea mataji yao katika mashindano yanayoendelea Mkoani Morogoro.

Mashindano hayo yaliyoanza wiki hii yalishuhudia timu ya Kandanda ya TPA ikiitembezea kichapo timu ya Chuo Kikuu Mzumbe kwa mabao 3 - 1, huku timu ya mpira wa kikapu ikiishiinda TRA kwa vikapu 52 - 25 na mechi iliyofuata ikaichabanga TRC vikapu 35 - 24.

Kwa upande wa Netiboli, timu ya TPA ambao ndio mabingwa watetezi imeifunga DIT 50  9 na BOT 52 - 10. Kwenye Mpira wa Wavu (Wanawake) timu ya TPA iliishinda NEMC kwa seti 2 - 0 na TANESCO kwa seti 2 -1.

Kwa upande wa mchezo wa kuvutana kwa Kamba,Timu ya TPA (wanaume) imecheza na timu za NIDA, NIT na SIDO na kushinda mechi zote kwa mivuto miwili kwa sufuri. Timu ya Wanawake nayo vile vile imeshinda michezo yake yote mitatu dhidi ya Mzinga,TSLB na MUHAS.