Sélectionnez votre langue

Baraza Dogo la Majadiliano la Bandari ya Dar es Salaam limewaaga wastaafu wawili baada ya kumaliza muda wao wa Utumishi kwa mujibu wa Sheria katika hafla fupi iliyofanyika mjini Bagamoyo.

Wastaafu hao ni pamoja na aliyekuwa Meneja wa Bandari kavu ya Ubungo na  Kwala Bw. Gabriel Mwangosi pamoja na aliyekuwa Mjumbe wa Baraza hilo Bi Modesta Kaunda.

Aidha Hafla hiyo ilitanguliwa na Kikao cha kwanza (1) cha Baraza Dogo la Majadiliano Bandari ya Dar es Salaam  kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

Baraza hilo limeongozwa na Meneja Zimamoto na Usalama Bw.Mussa Biboze kwa niaba ya Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Abed G.Abed.