Sélectionnez votre langue

Bandari ya Mtwara imefanya kikao chake cha thelathini na nane (38) cha Baraza la Wafanyakazi, tarehe 13 Novemba 2025 Mkoani Lindi.

Kikao hicho kimeongozwa na Meneja wa Bandari ya Mtwara Bw. Ferdinand S. Nyathi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo.

Lengo kuu la kikao hicho ni kujadili masuala mbalimbali yanayohusu utendaji kazi wa Bandari ya Mtwara ikiwemo mipango na mikakati ya maendeleo ya Bandari, mapato na matumizi, uhudumiaji wa shehena na meli pamoja na masuala mengine muhimu ya kiutawala na kiutendaji.

Kikao hicho kimefanyika kwa mafanikio makubwa ambapo wajumbe walipata fursa ya kujadili na kutoa maoni yenye lengo la kuboresha zaidi huduma na ufanisi wa Bandari ya Mtwara.

Kupitia majadiliano hayo, Baraza limeazimia kuendelea kushirikiana kwa karibu katika utekelezaji wa mikakati inayolenga kuinua tija na kuongeza mchango wa Bandari ya Mtwara katika kukuza uchumi wa Taifa.