Sélectionnez votre langue

Wafanyakazi Bandari ya Dar es Salaam waaswa kudumisha utulivu na kuhamasisha amani kwa kuwa Bandari ni sehemu nyeti na pia ni muhimili wa Uchumi katika kuingiza mapato nchini.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Abed G. Abed, tarehe 20 Disemba 2025 wakati akufungua Kikao cha kwanza cha Baraza la Wafanyanyakazi Kituo cha Bandari ya Dar es Salaam kilichofanyika mjini Bagamoyo Mkoa wa Pwani.

Amesema kuwa Watumishi wa Umma wanapaswa kuwa wa kwanza Katika kuhamasisha amani nchini hususan katika Bandari ya Dar es Salaam kwa kuwa ni sehemu nyeti hivyo wanatakiwa kujiepusha na mambo ya uvunjifu wa amani huku wakihakikisha wanadumisha utulivu ili kuifanya Bandari kuwa salama, ikiendesha shughuli zake na kuchangia katika kuongeza mapato ya Taifa.

 Aidha amekipongeza Chama cha Wafanyakazi wa Shughuli za Meli na Bandari Tanzania (DOWUTA kwa kuwa kiungo imara katika kuunganisha Menejimenti na Wafanyakazi pamoja na kushirikiana na Menejimenti katika kipindi chote na kuahidi kuendelea kudumisha ushirikiano na DOWUTA pamoja na Wafanyakazi wote.

Pamoja na mambo mengine Baraza hilo limewaaga wajumbe wake ambao wamemaliza muda wao wa utumishi kisheria ambao ni Bi. Hilder Mwakatobe, Bi. Modesta Kaunda, Bw. Mohamedi Telela, Bi. Celina Simon na Bi Brigita Madolomani