Select your language

Rais wa Malawi Mhe. Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera, ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa kuendelea kutoa huduma bora na za kuaminika za kibandari kwa mizigo na shehena zinazoingia na kutoka nchini Malawi kufuatia maboresho makubwa yanayoendelea katika Bandari ya  Dar es Salaam.

Mhe. Dkt. Chakwera ametoa pongezi hizo alipotembelea Banda la Maonesho la TPA, katika Sherehe za Ufunguzi wa Maonesho ya 35 ya Biashara ya Kimataifa ya Malawi (35th Malawi International Trade Fair) zilizofanyika Mei 23,2025 katika Viwanja vya Chichiri Jijini Blantyre, Malawi. 

TPA imeshiriki maonesho hayo kwa kishindo kikubwa kwa msisitizo wa huduma bora na za kuaminika kwa wateja wa TPA nchini Malawi.

Akiwa katika Banda la Maonesho la TPA,  Mhe. Dkt. Chakwera alipata maelezo ya shughuli mbalimbali za kibandari yaliyotolewa na Afisa Mwakilishi wa TPA Nchini Malawi Bw. Rex Suleiman na kupokea zawadi mahsusi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bw. Plasduce Mkeli Mbossa.

Get In Touch

For any inquiries or support, contact us 24/7
0800-110032
P.O Box 9184 Dar es salaam
dg@ports.go.tz
255 22 2130390

News & Updates Malawi

RAIS WA MALAWI ATEMBELEA BANDA LA MAONESHO LA TPA KATIKA MAONESHO YA...

26 May 2025

Rais wa Malawi Mhe. Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera, ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa kuendelea kutoa huduma bora na za kuaminika za kibandari kwa mizigo na shehena zinazoingia na kutoka nchini Malawi...
  Tell Me More
WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI ATEMBELEA OFISI...

07 March 2025

Matukio mbalimbali katika Picha wakati Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, alipotembelea Ofisi ya TPA Jijini Lilongwe nchini Malawi hivi karibuni. Mhe. Balozi Kombo, ameipongeza Mamlaka ya...
  Tell Me More