Mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania (TPA), imetoa msaada wa mashine mbili za incubator kwaajili ya kusaidia kuhifadhi watoto njiti zenye thamani ya Sh milioni 25 katika Hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Tanga. Akikabidhi msaada huo Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA Mhandisi Witonde Philipo, amesema kuwa mamlaka hiyo ilikuwa imetenga bajeti ya Sh milioni 50 kwa ajili ya kusaidia jamii katika sekta ya elimu na afya.