KATIKA PICHA NI MATUKIO MBALIMBALI KUHUSIANA NA ZIARA YA WANACHAMA WA BANDARINI SACCOS WALIPOTEMBELEA MRADI WA MABWAWA YA SAMAKI KIGAMBONI, ZIARA HIYO ILIFANYIKA MWEZI MACHI, 2019!

Picha 5

Picha 2

Picha 3

Picha 9

Picha 10

Pic 3

Mmoja wa Wafanyakazi wa TPA, Bi. Hilda Mwakatobe akikabidhi kwa mmoja wa wa Wazazi wa Watoto wagonjwa, Bi. Bi. Cheusi Selemani misaada mbalimbali kwa ajili ya watoto wao ambao wamezaliwa wakiwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi. Msaada huo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani Machi 8, 2019. Misaada hiyo imetolewa na Wafanyakazi Wanawake wa TPA ikiwa ni sehemu ya kusaidia jamii hususani kuwafariji wazazi wa watoto hao.

Pic 2

Mmoja wa Wafanyakazi wa TPA, Bi. Zahara Malika akikabidhi kwa Muuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Bi Rehema Ally misaada mbalimbali kwa ajili ya watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani Machi 8, 2019. Misaada hiyo imetolewa na Wafanyakazi Wanawake wa TPA ikiwa ni sehemu ya kusaidia jamii hususani kuwafariji wazazi wa watoto hao.

Pic 4

Baadhi ya wanawake ambao ni wafanyakazi wa TPA wakiwasili katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha Moi kwa wazazi wenye watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi ili kuwatembelea na kuwapa misaada ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.

Pic 5

Mkurugenzi wa Fedha wa TPA, Bi. Nuru Mhando (wapili kushoto) akimbeba mmoja wa watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi waliolazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha Moi mara baada ya kuwakabidhi misaada mbalimbali ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.

Pic 6

Baadhi ya Wanawake ambao ni Wafanyakazi wa TPA wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi misaada mbalimbali ikiwa ni pamoja na juice, biskuti, soda na fedha taslimu kwa ajili ya kulipia bima ya afya ya NHIF kwa watoto 20 wenye watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (MB) hivi karibuni amekutana na Wafanyabiashara wa DRC kwa lengo la kupatia ufumbuzi changamoto ya kukwama kwa kontena za Wafanyabiashara hao zaidi ya 900 katika Bandari ya Dar es Salaam.

Waziri Kamwelwe amekutana na baadhi ya wawakilishi wa Wafanyabiashara hao jijini Dar es Salaam hivi karibuni na kutatua changamoto zote ambazo zilisababisha kwa namna moja au nyingine kutolewa kwa kontena hizo.

Baada ya kupata ufumbuzi tayari kontena hizo zimeanza kuondolewa ndani ya Bandari tangu Februari 18, 2019.

KATIKA PICHA NI MATUKIO MBALIMBALI KUHUSIANA NA KIKAO HICHO:

41

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (MB) akifafanua jambo mbele ya Wafanyabishara  kutoka Congo DRC (hawapo pichani) katika kikao kazi kilicholenga kutafuta ufumbuzi wa kukwama kwa makontena zaidi ya 900 ndani ya Bandari ya Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Balozi wa Congo nchini Tanzania, Mhe. Yamba Yamba.

32

Baadhi ya Wafanyabiashara kutoka Congo DRC wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (MB) katika kikao kazi kuhusu kukwama kwa kontena zaidi ya 900 Bandari ya Dar es Salaam kilichofanyika Jijini Dar es Salaam, ambapo Serikali imeanza kuruhusu makontena hayo kuanza kutolewa leo Februari 18, 2019.

22

Kaimu Balozi wa Congo nchini Tanzania Yamba Yamba (kulia) akimsikiliza, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (MB) katika kikao kazi kuhusu kukwama kwa makontena zaidi ya 900 katika Bandari ya Dar es Salaam, kilichofanyika Jijini Dar es Salaam, ambapo Serikali imenza kuruhusu makontena hayo kuanza kutolewa leo Februari 18, 2019.

12

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (MB) akisisitiza jambo mbele ya Wafanyabishara  kutoka Congo DRC katika kikao kazi kilichohusu kukwama kwa kontena zaidi ya 900 katika Bandari ya Dar es Salaam, kilichofanyika Jijini Dar es Salaam, ambapo Serikali tayari imenza kuruhusu kontena hizo kuanza kutolewa kuanzia Februari 18, 2019.

Capture 14

picha 1

Kaimu Mwenyekiti Baraza la Wafanyakazi Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Ahmed Mchalaganya (katikati) akiongea jambo wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi  Kamati ya Utendaji Kikao cha 61 Kamati ya Utendaji  Bandari ya Dar es Salaam kilichoanza kujadili tarifa ya Utekelezaji wa Malengo kwa Mwaka 2018/2019 kipindi cha Nusu mwaka Julai - Disemba, 2018 na Malengo mapya ya Mwaka 2019/2020 Bandari ya Dar es Salaam.

Picha 2

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Mashaka Karume akiongea jambo wakati wa kikao hicho cha kamati ya Utendaji Bandari ya Dar es Salaam.

Picha 3

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Bandari ya Dar es Salaam wakimksikiliza mtoa mada (hayupo pichani) wakati wa kikao cha 61 Kamati ya Utendaji Bandari ya Dar es Salaam kilichofanyika katika ukumbi wa Zimamoto na Usalama.

Picha 4

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Bandari ya Dar es Salaam wakimksikiliza mtoa mada (hayupo pichani) wakati wa kikao cha 61 Kamati ya Utendaji Bandari ya Dar es Salaam kilichofanyika katika ukumbi wa Zimamoto na Usalama.

Chuo cha Bandari kitaanza rasmi kudahili Wanafunzi wapya kupitia mfumo wake mpya wa kidijitali ujulikanao kama “Student’s Information Management System (SIMS)”.

 

Mfumo huo wa kidijitali umezinduliwa hivi karibuni na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaac Kamwelwe (MB) ambae amesema utakiwezesha Chuo kudahili wanafunzi wanaopenda kujiunga na Chuo kutumia njia ya mtandao.

 

Mfumo huo ambao umebuniwa na kutengenezwa na wafanyakazi wa TPA kitengo cha TEHAMA, pia utatumika kukokotoa matokeo ya mitihani na kuanda taarifa ya mwisho wa mwaka wa mafunzo yaani ‘final year transcript’.

 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tovuti ya mfumo huo mpya, Waziri Kamwelwe alisema uwepo wa mfumo huo utasaidia kudhibiti udanganyifu uliokuwa ukifanywa na baadhi ya watendaji wa Chuo wasiokuwa waaminifu.

 

Mhandisi Kamwelwe ameongeza kwamba awali wakati udahili ulipokuwa ukifanywa kwa kujaza fomu kwa mkono ‘manual’, kulikuwa na tatizo la uchakachuaji wa vyeti na upotevu wa pesa.

 

“Wakati wa kufanya maombi ya kujiunga na Chuo kwa kujaza nyaraka “application manual” kuna fomu za maombi zilikuwa zinapotea na kulikuwa na upotevu wa pesa pamoja na tatizo la kuchapisha vyeti feki na baadhi ya Wanafunzi kutohudhuria mafunzo ipasavyo,” amesema Waziri Kamwelwe.

 

Ameongeza kwamba katika kipindi hicho baadhi ya Wanafunzi waliishia kusajiliwa tu na baada ya miaka miwili unamkuta na cheti mtaani lakini sasa kwa kuwepo kwa mfumo huu ni matarajio yetu mambo hayo yatakwisha kabisa.

 

Kwa upande wake Mkuu wa Bodi ya Magavana ya Chuo na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko amemshukuru Waziri kwa kutenga muda wake na kuzindulia tovuti hiyo ambayo ni nyenzo muhimu kwa chuo katika kuongeza ufanisi na kuondoa mianya ya utendaji mbovu.

 

Mhandisi Kakoko amesema kwamba pamoja na ukweli kwamba Waziri ana mambo mengi lakini bado ameweza kutenga muda na kuthamini jitihada ambazo Mamlaka imezichukua katika kuimarisha utendaji wa Chuo cha Bandari husuani kuzindua mfumo huo muhimu kwa maslahi ya Chuo na Taifa kwa jumla.

 

“Uwepo wa mfumo huu, utarahisisha utendaji kazi wetu kama Chuo na kudhibiti wale wote waliokuwa wakitumia mianya ya kutokuwepo kwa mifumo hiyo, kufanya udanganyifu,” amesema Mhandisi Kakoko.

 

Akizungumzia faida za mfumo huo, mmoja wa wafanyakazi wa TPA ambaye ameshiriki kubuni mfumo huo, Bw. Rainer Mwashu amesema utarahisisha zoezi la udahili wanafunzi na kupata taarifa zao kwa urahisi wakati wowote zikihitajika.

 

“Kupitia mfumo huu, Mwanafunzi ataweza kujisajili kwa ajili ya mwaka wa masomo popote pale alipo…amesema na kuongeza kwamba,…kwa sasa taarifa zote za wanafunzi wa Chuo hiki zitapatikana kidijitali kupitia mfumo huu.”

 

Mbali ya hayo, mfumo huu pia utatumika kuzalisha taarifa ya mwisho ya matokeo ‘final year transcript’, na utawezesha kuoana kwa mifumo ya ndani na nje ya taasisi kama vile NACTE, NECTA na GePG.

Pic 4

Pic 1

Pic 2

Pic 3

 

 

Wabunge Watanzania kwenye Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki wametembelea Bandari ya Dar es Salaam Jumatatu, Februari 04, 2019 na kukutana na wadau mbalimbali wanaoshughulika na usafirishaji mizigo kutoka na kwenda kwenye nchi Wanachama wa Jumuiya.

Katika ziara yao hiyo Wabunge hao walipokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Elihuruma Lema kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Bandari ya Dar es Salaam, Eng. Deusdedit Kakoko. Wakiwa Bandarini hapo Wabunge hao pia walikutana na Uongozi wa Chama cha Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA) pamoja na Afisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

KATIKA PICHA NI MATUKIO MBALIMBALI KUHUSIANA NA ZIARA YA WABUNGE HAO.

DSC 0091

DSC 0121

DSC 0112

DSC 0084

DSC 0082

DSC 0070

DSC 0064

DSC 0054

 

Tanzania: World Bank Nods to Berth Construction At Dar Port

WORLD Bank has appreciated progress of the Dar es Salaam Maritime Gateway Project (DMGP), which is at 43 per cent of execution and expected to start operating early next year.

The project involves construction and rehabilitation of 12 berths, with the rehabilitation including deepening and strengthening of the docks.

WB Country Director Bella Bird, accompanied by other WB officials, yesterday visited the Dar es Salaam port, saying her office was satisfied with the project implementation.

"The work is going on well... we have observed that activities at the first berth are over and now the contractor has shifted to the second berth which we expected to see its accomplishment next month.

The contractor runs it in professional way and TPA is doing well," she noted. Tanzania Ports Authority (TPA) Director of Engineering Services, Engineer Charles Ogare clarified that the seven-year project (2017-2024) costs 420 million US dollars (over 990bn/), adding that at least eight berths will be accomplished within 36 months and the job will be done by 2020.

He said about 336bn/- was used in the first phase of the project, which included rehabilitation of seven berths and construction of the 'ro-ro berth' specifically for driving-off vehicles from vessels.

"We are therefore rehabilitating seven berths plus construction of the one for the vehicles, bringing the total of eight.

We expect to finish the work on time despite challenges we face, especially presence of unfit soil, which we have to take away and bring in the proper one.

It consumes time but we are doing our best to do the job as per schedule," he said. It was revealed that feasibility studies for the rest of the berths are on progress to let the whole DMGP to start operations by 2024.

Upon full operations, each berth is set to accommodate 70,000 tonnes ship with up to 300 meters' width. Currently, the berths accommodate 20,000 tonnes ships, according to Engineer Ogare.

Source: Read the original article on Daily News.

KATIKA PICHA NI MATUKIO MBALIMBALI KUHUSIANA NA ZIARA YA BENKI YA DUNIA BANDARINI

Pic 1

Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko (kushoto) akizungumza na ujumbe wa Benki wa Dunia (WB) ulioongozwa na Mkurugenzi Mkazi wa Benki hiyo hapa nchini, Bi. Bella Bird (kulia) mara baada ya kufanya ziara ya kikazi kukagua miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Benki hiyo ndani ya Bandari.

Pic 2

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uhandisi, Mhandisi Charles Ogare (wa tatu kushoto) akiongozana na ujumbe wa wageni kutoka Benki ya Dunia (WB), ulioongozwa na Mkurugenzi Mkazi wa Benki hiyo, Bi. Bella Bird (wa pili kulia) mara baada ya kufanya ziara Bandari ya Dar es Salaam kukagua mradi wa maboresho ya Bandari hiyo.

Pic 5

Mkandarasi toka kampuni ya ujenzi ya China Habour Engineering (CHEC) akitoa maelezo kuhusiana na maendeleo ya ujenzi wa mradi wa maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam kwa ujumbe wa wageni kutoka Benki ya Dunia (WB), ulioongozwa na Mkurugenzi Mkazi wa Benki hiyo, Bi. Bella Bird (katikati) mara baada ya kufanya ziara Bandari ya Dar es Salaam kukagua maendeleo ya mradi wa maboresho ya Bandari hiyo.

Pic 31

Mkandarasi toka kampuni ya ujenzi ya China Habour Engineering (CHEC) akitoa maelezo kuhusiana na maendeleo ya ujenzi wa mradi wa maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam kwa ujumbe wa wageni kutoka Benki ya Dunia (WB), ulioongozwa na Mkurugenzi Mkazi wa Benki hiyo, Bi. Bella Bird (katikati) mara baada ya kufanya ziara Bandari ya Dar es Salaam kukagua maendeleo ya mradi wa maboresho ya Bandari hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko tarehe 26 na 27 Januari, 2019 amekutana na kufanya mikutano na Wadau wa bandari katika Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha

Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mkutano na wadau wa bandari wa Mkoa wa Arusha, Mhandsi Kakoko amesema kuwa lengo la kukutana na wadau hao ni kuwafahamisha maboresho mbalimbali yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika katika bandari ya Tanga na kuifanya bandari hiyo kutoa huduma bora zaidi

Mhandisi Kakoko aliongeza TPA inalenga kutumia mikutano na wadau kupata mrejesho ya huduma zinazotolewa na bandari na maeneo gani huduma zinapaswa kuboreshwa

Katika kutatua changamoto zilizotolewa na wadau hao, Mhandisi Kakoko amesema kuwa changamoto ambazo zipo ndani ya uwezo wa TPA zitapatiwa ufumbuzi mara moja na zile ambazo zinahusu taasisi nyingine kama TRA,TBS, n.k atashirikisha watendaji wakuu wa taasisi hizo ili kuhakikisha mteja anayepita na kutumia bandari za Tanzania anapata huduma bora zinazolenga kumpunguzia mteja gharama ya kufanya biashara.

Kwa upande wake Meneja bandari ya Tanga Bw Percival Salama amewataka Wadau hao kutumia bandari ya Tanga katika kupitisha mizigo yao kutokana na kuhudumia wateja kwa kasi kubwa na haraka zaidi pamoja na kuwa na vifaa vipya vya kupakia na kupakua mizigo .

Mkutano wa wadau katika Mkoa wa Arusha ulifunguliwa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Mrisho Gambo na ule wa Mkoa wa Kilimanjaro ulifunguliwa na Katibu Tawala wa Mkoa Mhe.Mhandisi Aisha Amour.

WADAU

WADAU 1

WADAU 2

WADAU 3

WADAU 4

WADAU 5

WADAU 6

WADAU 7

WADAU 8