DAR PORT TO START SERVING MALAWI CARGO BY 100 PERCENT!

Minister for Works, Transport and Communications, Eng. Isack Kamwelwe (MP) has called on Tanzania Ports Management Authority (TPA) to start serving Malawi cargo by 100 percent from now.

The Minister has made the ruling on Friday, March 29 during a joint session meeting held in Dar es Salaam recently with the Minister of Transport and Construction of Malawi, Hon. Jappie Mhango (MB).

BANDARI YA DAR ES SALAAM KUANZA KUHUDUMIA SHEHENA YA MZIGO WA MALAWI KWA ASILIMIA 100!

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (MB), ameiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kujipanga kuhudumia shehena ya mzigo wa Malawi kutoka asilimia 20 hadi 100 kuanzia sasa.

Waziri Kamwelwe ametoa agizo hilo Ijumaa, Machi 29 wakati wa kikao cha pamoja baina yake na Waziri wa Uchukuzi na Ujenzi wa Malawi, Mhe. Jappie Mhango (MB) kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

“Hivi karibuni kumetokea mvua kubwa ambazo zimesababisha uharibifu mkubwa kwenye Bandari ya Beira nchini Msumbiji pamoja nan chi ya Malawi ambayo awali ilikuwa ikiitumia Bandari hiyo kupitishia mzigo wa Malawi, kutokana na uharibifu huo sasa Malawi wataitumia Bandari ya Dar es Salaam kwa asilimia 100 badala ya asilimia 20 ya awali,” amefafanua Waziri Kamwelwe.

Waziri amesema kwamba Bandari ya Beira kwa sasa imeoshwa kabisa na mafuriko yaliyotokea na jambo hilo sasa linaifanya Malawi kuanza kutumia Bandari za Tanzania hususani Bandari ya Dar es Salaam kwa asilimia mia moja.

Pamoja na hilo Waziri Kamwelwe amesema maamuzi ya kutumia Bandari za Tanzania pia yametokana na mazungumzo ambayo ameyafanya na Waziri mwenzake wa Malawi yaliyolenga kuimarisha mahusiano ya kibiashara baina ya nchi za Tanzania na Malawi.

Ameongeza kuwa mkutano wake na Waziri mwenzake pia umelenga kuona mahusiano baina ya nchi hizi mbili yalianza wapi na wapi wanaweza kuboresha na wamegundua kuwa tayari kulikuwa na mkataba wa mahusiano kati ya Tanzania na Malawi ambao ulisainiwa na Mawaziri wa Uchukuzi mwaka 1987.

“Bahati nzuri tumeupata na tumeupitia mkataba huo wa mahusiano ambao kimsingi ndio uliifanya Serikali ya Malawi ikajenga Bandari kavu ambazo leo zinazojulikana kama Malawi Cargo hapa Dar es Salaam na Mbeya,” amefafanua Waziri.

Amesema kuwa ili kuendelea na utekelezaji wa mkataba huo wamekubaliana kuunda timu ambayo itapitia mkataba huo ambao kimsingi haujawahi kufanyiwa marekebisho ili uweze kukidhi matakwa ya sasa ya kisheria, taratibu na kanuni kwa lengo la kuingiza mabadiliko yatakayokidhi mahitaji ya sasa ya kijamii na kibiashara.

Mhandisi Kamwelwe ameongeza kuwa katika kutekeleza mkataba huu Mawaziri watakuwa wakikutana kila baada ya miezi sita ili kujadili mambo ya kibiashara na kwa kuanzia tayari amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko kujipanga kuhudumia nyongeza ya shehena ya mzigo kutoka Malawi kwa asilimia 100.

“Ni lazima mjipange ili kuhakikisha mzigo unapitia kwa haraka katika muda wanaotaka wateja wa Malawi na kwa bahati nzuri kwenye Bandari Kavu za Malawi kuna miundombinu mingi mpaka matanki ya mafuta hivyo ni matumaini yetu kwamba mzigo utaongezeka,” ameongeza Waziri.

Sambamba na hilo Waziri amebainisha kwamba Serikali itahakikisha kwamba mahusiano ya kibiashara na kijamii baina ya Tanzania na Malawi yanakuwa makubwa na ili kutekeleza hilo wamejipanga kufanya kikao kingine tarehe 14 Juni 2019 jijini Dar es Salaam.

Inatarajiwa kwamba timu ya wataalamu mbalimbali kama vile Wanasheria, Wataalamu wa Biashara na Maafisa Mipango watapitia makubaliano ya mwaka 1987 na kuweza kuona endapo kuna haja ya kubadili kidogo baadhi ya vifungu vya makubaliano ili kuviboresha na kuendana na hali ya sasa hivi.

Kwa upande wake Waziri wa Uchukuzi wa Malawi Mhe. Mhango amesema wanaishukuru sana Serikali ya Tanzania kwa undugu mkubwa waliouonesha kwa Wananchi wa Malawi na hasa katika kuwapatia msaada mkubwa wa madawa na chakula kwa waathirika wa mafuriko.

“Napenda kumshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. John Pombe Joseph Magufuli, Waziri mwezangu na Baraza lote la Mawaziri kwa mchango wao mkubwa kwa Serikali ya Malawi hususani kwa msaada wa chakula na madawa na tunaamini kwamba mambo mengine ya kibiashara tuliyoyajadili yatafanyiwa kazi na kupata ufumbuzi wa kudumu,” amehitimisha Mhe. Mhango.

KATIKA PICHA NI MATUKIO MBALIMBALI KUHUSIANA NA MKUTANO HUO:

PIC 1

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (MB) akizungumza na Wajumbe wa kikao chake na Waziri wa Uchukuzi na Ujenzi wa Malawi, Mhe. Jappie Mhango (MB) (wapili kushoto).

PIC 2

PIC 3

PIC 4

PIC 5

PIC 6

PIC 7

PIC 8