Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (MB) hivi karibuni amekutana na Wafanyabiashara wa DRC kwa lengo la kupatia ufumbuzi changamoto ya kukwama kwa kontena za Wafanyabiashara hao zaidi ya 900 katika Bandari ya Dar es Salaam.

Waziri Kamwelwe amekutana na baadhi ya wawakilishi wa Wafanyabiashara hao jijini Dar es Salaam hivi karibuni na kutatua changamoto zote ambazo zilisababisha kwa namna moja au nyingine kutolewa kwa kontena hizo.

Baada ya kupata ufumbuzi tayari kontena hizo zimeanza kuondolewa ndani ya Bandari tangu Februari 18, 2019.

KATIKA PICHA NI MATUKIO MBALIMBALI KUHUSIANA NA KIKAO HICHO:

41

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (MB) akifafanua jambo mbele ya Wafanyabishara  kutoka Congo DRC (hawapo pichani) katika kikao kazi kilicholenga kutafuta ufumbuzi wa kukwama kwa makontena zaidi ya 900 ndani ya Bandari ya Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Balozi wa Congo nchini Tanzania, Mhe. Yamba Yamba.

32

Baadhi ya Wafanyabiashara kutoka Congo DRC wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (MB) katika kikao kazi kuhusu kukwama kwa kontena zaidi ya 900 Bandari ya Dar es Salaam kilichofanyika Jijini Dar es Salaam, ambapo Serikali imeanza kuruhusu makontena hayo kuanza kutolewa leo Februari 18, 2019.

22

Kaimu Balozi wa Congo nchini Tanzania Yamba Yamba (kulia) akimsikiliza, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (MB) katika kikao kazi kuhusu kukwama kwa makontena zaidi ya 900 katika Bandari ya Dar es Salaam, kilichofanyika Jijini Dar es Salaam, ambapo Serikali imenza kuruhusu makontena hayo kuanza kutolewa leo Februari 18, 2019.

12

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (MB) akisisitiza jambo mbele ya Wafanyabishara  kutoka Congo DRC katika kikao kazi kilichohusu kukwama kwa kontena zaidi ya 900 katika Bandari ya Dar es Salaam, kilichofanyika Jijini Dar es Salaam, ambapo Serikali tayari imenza kuruhusu kontena hizo kuanza kutolewa kuanzia Februari 18, 2019.