
BODI YA WAKURUGENZI WA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI TANZANIA YATEMBELEA BANDARI YA MTWARA
- MKANDARASI WA UJENZI WA GATI AHIMIZIWA KUMALIZA KAZI KWA WAKATI
Bodi ya wakurugenzi ikiongozwa na Mwenyekiti wake Prof. Ignas Rubaratuka imetembelea Bandari ya Mtwara tarehe 12-13.09.2019 kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo pamoja na ujenzi wa gati moja unaoendelea.
Bodi hiyo ilipata fursa ya kutembelea mradi wa ujenzi wa gati ambapo wameishauri Menejimenti ihakikishe kwamba inasimamia kwa karibu mradi huo ili uweze kumalizika kwa wakati.
Mradi huo uliwekwa jiwe la msingi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. John Pombe Joseph Magufuli tarehe 04 Machi, 2017 ambapo ulitarajiwa kukamilika tarehe 31 Agosti, 2019 lakini umeshindwa kukamilika kwa wakati kutokana na sababu mbalimbali zilizojitokeza ikiwemo kuwepo kwa udongo usiofaa ambao ulihitajika kuchimbwa kabla ya kuanza ujenzi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko ameieleza Bodi kwamba Menejimenti imejipanga vizuri kusimamia mradi huo kwa karibu na wataendelea kushirikiana na Mhandisi mshauri wa Mradi huo ili kuhakikisha kwamba mradi huo unakamilika kwa ufanisi.
Wafuatao wamefaulu usaili na kufanikiwa kuajiriwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania, hivyo mnatakiwa kufika Ofisi za Makao Makuu ya TPA zilizopo katika jengo la Bandari Tower ghorofa ya 32 kuchukua barua za Ajira.
Matukio mbalimbali katika picha kuhusiana na Kikao cha Ishirini na nane (28) cha Kamati ya Utendaji ya Baraza kuu la Wafanyakazi la TPA, kinachofanyika katika Chuo cha Afya mjini Bagamoyo. Kikao hicho kimefunguliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, Eng. Deusdedit Kakoko.