Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imejipanga kuhudumia shehena ya mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda pindi uzalishaji wa bidhaa hiyo utakapoanza rasmi mwaka 2025.
Tanzania ilishinda tenda ya kupitisha mafuta ghafi kwa njia ya bomba kutoka mji wa Hoima yanapozalishwa hadi kwenye masoko ya nje kupitia Bandari ya Chongoleani mjni Tanga
.
Uamuzi wa Mwisho wa Uwekezaji wa miradi ya juu na EACOP ulitangazwa tarehe 1 Februari, 2022 na maendeleo ya mradi yanaendelea kwa lengo la Mafuta ya Kwanza mwaka 2025.
Haya yalisemwa hivi karibuni na Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano, Dkt. George Fasha wakati wa mkutano na maonyesho ya 10 wa Mafuta ya Afika Mashariki uliofanyika Nchini Uganda.
Dkt Fasha ambaye alikuwa ni mmoja wa wasilishaji mada katika mkutano huo, alisema TPA kupitia Bandari yake ya Chongoleani iliyopo mjini Tanga, imejipanga kuhudumia shehena hiyo kwa ufanisi mkubwa.
Amesema kwamba Bandari ni Lango la Biashara, Kitaifa na Kimataifa, hivyo kama ikitumiwa ipasanvyo itafungua milango ya biashara na maendeleo ya kiuchumi kwa nchi za Afrika Mashariki.
“Ili kufanikisha haya, tuna mradi mkubwa wa kimkakati unaojulikana kama DMGP ambao umejikita katika kufanya maboresho ya kimiundombinu kwa Bandari ya Dar es Salaam,” alisema Dkt. Fasha.
Mradi huu unahusisha pamoja na mambo mengine, maboresho ya kiutendaji kwa wafanyakazi wetu ambao wamepatiwa mafunzo mablimbali ya jinsi ya kuhudumia meli na mizigo inayopita Bandari ya Dar es Salaam na zinginezo.
Mkutano huo uliolenga kuionyesha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kama kimbilio la chaguo la fursa za uwekezaji wa mafuta na gesi ili kuboresha mageuzi ya kijamii na kiuchumi.
Bandari ni lango la biashara na kama ikitumiwa ipasanvyo itafungua mialngo la biashara na maendeleo ya kiuchumi.
Ili kufanikisha haya, tuna mradi mkubwa wa kimkakati ujulikano kama DMGP ambao lengo lake ni kufanye maboresho ya kimiundombinu kwa Bandari ya DSM
Mradi huu unahusisha Pamoja na mambo mengine pia na maboreho ya kiutendaji wa wafanyakazi wetu ambapo wamewezeshwa kwa kupata mafunzo mablimbali ya jinsi ya kuhdumia meli na mzigo inayopita Bandarini.
Mwisho