Na Leonard Magomba

Bw. Mrisho Mrisho ameteuliwa kushika nafasi ya Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Juma Kijavara ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Mrisho aliwahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi katika TPA (Mamlaka ya Usimamzi wa Bandari Tanzania) akianzia na nafasi ya Mkuu wa Ulinzi na Usalama wa Bandari ya Mtwara.

Mara baada ya kuhudumu katika nafasi hiyo kwa miongo kadhaa, Bw. Mrisho alipandishwa cheo na kuwa Msaidizi wa Mkurugenzi Mkuu wa TPA kwa miongo kadhaa.

Bw. Mrisho aliteuliwa kushika nafasi ya Meneja wa Ulinzi na Usalama wa Bandari ya Dar es Salaam, kabla ya kuteuliwa kushika nafasi ya Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam.

Mwisho