Na Leonard Magomba

Bw. Plasduce Mkeli Mbossa ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na kuchukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Bw. Eric Hamissi.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Mbossa aliwahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi katika Mamlaka hiyo, ikiwemo ya Meneja Mratibu wa Bandari zilizo chini ya Mamlaka.

Mara baada ya kuhudumu katika nafasi hiyo kwa miongo kadhaa, Bw. Mbossa alipandishwa cheo na kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA.

Bw. Mbossa aliteuliwa kushika nafasi ya Mkurugenzi Mkuu kutokea nafasi aliyokuwa akitumia Naibu Mkurugenzi Mkuu.

Ikumbukwe kwamba kabla ya teuzi zote hiyo, Bw. Mbossa aliwahi kuhudumu kama Msaidizi wa Mkurugenzi Mkuu wa TPA kwa miongo kadhaa.

Mwisho