MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI TANZANIA

TANGAZO:

  1. Ndugu Wananchi mnatangaziwa kuwa siku ya Jumamosi tarehe 23/11/2019, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), itasafirisha mzigo wenye vipimo vikubwa kutoka Bandari ya Dar es Salaam kuelekea Bandari ya Tanga. Gari litakalotumika kusafirisha mzigo husika limesajiliwa kwa namba: SU 43069/SU 41437.
  1. Gari hilo lina vipimo vifuatavyo:

 

  • Urefu - mita 18.80
  • Upana - mita 3.75
  • Kimo - mita 4.50
  1. Barabara zitakazotumika:
  • Mandela/SamNujoma/Bagamoyo/Msata-Segera/Segera-Tanga
  1. Gari litasafiri kuanzia saa 12:30 asubuhi mpaka saa 12:00 jioni.

Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Imetolewa na:

Menejimenti

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania-TPA

MAKAO MAKUU