Jumla ya maofisa 44 kutoka Chuo Cha Kijeshi kilichopo Duluti Arumeru Mkoani Arusha wametembelea Bandari ya Tanga kwa lengo la kujifunza na kuona utendaji wa Bandari. Akiongea kwa niaba ya Maafisa hao, Mkuu wa msafara huo, Kanali W. Mwamunyange alibainisha kuwa lengo la ziara hiyo ni kujifunza na kuona shughuli zinazofanywa na Bandari. Amengeza kuwa mbali ya hiyo, ziara hiyo pia inawasaidia kujenga uhusiano mzuri katika ulinzi na usalama kwenye maeneo mbalimbali ya mipaka ya Tanzania. Maafisa hao ni wanafunzi wanaotoka katika nchi za Tanzania, Burundi, Rwanda, Zambia, Zimbabwe, Malawi, Nigeria, Kenya, Misri na India. Sehemu ya maofisa 44 kutoka Chuo Cha Kijeshi kilichopo Duluti Arumeru Mkoani Arusha wametembelea Bandari ya Tanga Baadhi ya maofisa 44 wa kijeshi wakiwa Bandari ya Tanga Maofisa 44 kutoka Chuo Cha Kijeshi kilichopo Duluti Arumeru Mkoani Arusha wakiwa katika picha ya pamoja Mwisho